
Chanzo cha picha, AFP
Wanajeshi wa AMISOM Somalia
Kikosi cha wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika nchini Somalia, kimekabidhi kambi tatu kwa jeshi la Somalia kama sehemu ya hatua ya kuanza kuwaondoa wanajeshi wote wa Umoja huo.
Chini ya mpango huo, Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS), kitaondoa wanajeshi elfu mbili ifikapo kesho tarehe 30 Juni kutoka katika kambi zake za Somalia.
Shughuli hizi za kuondoa wanajeshi ni kwa mujibu wa ratiba ambayo Somalia na washirika wake wa kiulinzi na kiusalama wamekubaliana.
Itakumbukwa kuwa AMISOM imekuwa Somalia kuanzia, 2007 kabla ya hapo mwaka 2006 kulikuwa na kikosi cha nchi za pembe mwa Afrika - IGAD. AMISOM imekuwepo mwaka huo hadi mwezi wa nne mwaka jana kabla ya kubadili jina - ATMIS.
Somalia inaweza kujisimamia?
Bado Al-shabaab ni kitisho kwa nchi ya Somalia na majirani zake. Hivi karibuni kundi hilo la kigaidi limevamia kambi ya wanajeshi kutoka Uganda, eneo la Buulo Mareer kusini magharibi mwa mji wa Mogadishu. Wanajeshi wapatao 54 waliuwawa.
Siku chache baadaye, Jumapili ya Juni 25 kundi hilo lilifanya mashambulizi katika vijiji viwili huko Lamu, Kenya. Taarifa zinaeleza watu watano waliuwawa, nyumba zilichomwa na mali kuharibiwa.
Nguvu za Al shabab kufanya mashambulizi ndani ya Somalia na nje bado ni kubwa. Ndipo swali wengi wanajiuliza, ikiwa nchi hiyo inao uweo wa kuzuia wapiganaji hao wasifanye mashambulizi ndani na nje.
“Kwa mujibu wa ATMIS na AMISOM na vikosi vingine vya usalama - vikosi vya usalama vya Somalia vimeimarishwa. Sioni kuondoka kwa ATMIS kutaleta changamoto za kiusalama. Na hata kama kutakuwa na changamoto hazitokuwa kubwa,” anasema mwandishi mwandamizi wa kitendo cha Fastestsmm Monitoring, Samuel Murunga.
Somalia imeongoza juhudi za kuwapa mafunzo wanajeshi wake, wale wapya ambao wameingia katika jeshi la nchi. Na kuunda vikosi maalumu ya kupambana na uhalifu wa Alshabab. Kuna taarifa zinaeleza wanajeshi wao wanapokea mafunzo Urusi, Ehiopia, na Uganda. Vilevile wengine watapewa mafunzo maalumu ya kupambana na Al shabab katika nchi za Kenya na Djibouti.
Kando na vikosi vya ATMIS, Ethiopia ina wanajeshi ambao wanaendelea kuhusika na shughuli za kusaidia wanajeshi wa Somalia kulinda nchi na kupigana na Al-shabab. Na vikosi hivyo haviko chini ya usimamizi wa ATMIS. Na hakuna taarifa Hadi sasa kuwa wanajeshi wa Ethiopia wataondoka.
Licha ya hayo yote, mjadala kuhusu uwezo wa Somalia kujisimamia na kujilinda dhidi ya mashambulizi ya Al-shabab utaendelea kuwepo. Na kwa hakika si kazi rahisi kupambana na kundi la muda mrefu lenye uwezo wa kijeshi. Mjadala juu ya uwezo wa Somalia dhidi ya Al-shabab ni jambo la kusubiri na kuona.
Chanzo cha picha, Getty Images
Wapiganaji wa Alshabab
Changamoto
Kwa muda mrefu Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa liliwekea vikwazo vya silaha Somalia. Ikiwa nchi hii itaendelea kubaki katika vikwazo, yamkini mpango wake wa kukabiliana na Al shabab utaathrika.
Lakini mchambuzi wa masuala ya kiusalama, Richard Tuta ana matumaini chanya kuhusu vikwazo hivyo. Ameimbia Fastestsmm:
"Kulikuwa na sababu ya barala la usalama la Umoja wa Mataifa kuiwekea Somalia vikwazo vya kununua silaha, kuondoka kwa ATMIS huenda hizo sababu zisiwepo tena, kwa sababu vyombo vya dola vya Somalia vitakuwa huru, huenda wakaweza kuruhusiwa kujisimamia na kujinunulia silaha."
Jukumu la Vikosi vya Afrika limefikiwa?
Kwa mujibu wa mpango huo zile sehemu ambazo zimekuwa zikisimamiwa na walinda amani wa Afrika hazitaachwa wazi. Badala yake zitasimamiwa na wanajeshi na vyombo vya usalama wa Somalia.
Al-shabab bado nguvu ya kushambulia, bado Ina wanachama, ina silaha na inadhibiti baadhi ya maeneo ndani ya Somalia. Je, jukumu la walinda amani wa Afrika limefanikiwa?
"Kwanza tunapaswa kujiuliza; jukumu lao la kuwa kule walilkuwa wanatarajiwa kufanya nini? Cha umuhimu walichokuwa wanatarajiwa kufanya – kwanza ni kulinda sehemu za kimkakati. Moja wapo ni bandari, uwanja wa ndege, Bunge la nchi ma kuhakikisha misaada inafikia wanaohitaji. Utaona hayo yote yamefanhyika," anasema Richard Tuta.
Anaongeza Kwa kusema, "la umuhimu pia, ilikuwa ni kuweza kuwafunza vikosi vya usalam vya nchi ya Somalia na sio wanajeshi tu, bali pia Polisi, na kikosi cha ujasusi cha nchi hyo, hayo yote wameweza kuyafanya."