Kipi tunakijua kuhusu mkutano wa Putin na mkuu wa Wagner baada ya uasi? - Fastestsmm News Swahili
Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha,
Vinyago vya uso vinavyoonyesha mkuu wa Wagner Yevgeny Prigozhin na Rais wa Urusi Vladimir Putin vinauzwa katika soko la ukumbusho huko St Petersburg mwezi uliopita.
Siku tano baada ya uasi wa mamluki wa Wagner wakiongozwa na Yevgeny Prigozhin, mkutano umefanyika kati yake na Rais wa Urusi Vladimir Putin, kulingana na kauli ya kile Kremlin.
Hebu tuende moja kwa moja kwenye habari yenyewe. Asubuhi ya Juni 24, siku ya uasi, Putin alimsuta kiongozi wa Wagner kwa uhaini na usaliti. Baadaye mchana, wapiganaji wa Wagner waliangusha ndege za Jeshi la Wanahewa la Urusi, na kuwaua marubani wawili.
Baada ya hapo, wakati mamluki wa Wagner wakiwa kilomita 200 tu kutoka mji mkuu, Moscow, Kremlin iliingia makubaliano na mamluki hawa, kukomesha uasi, bila kumkamata mtu yeyote, wala kumwajibisha mtu yeyote kisheria.
Kwa maana hiyo, Yevgeny Prigozhin hakutiwa pingu, wala hakukamatwa kama adhabu ya uasi wake.
Leo, mkutano ambao ulifanyika kati ya Prigozhin na viongozi wenzake wa Wagner kwa upande mmoja na Rais Putin umefanyika huko Kremlin.
Msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov alithibitisha kwamba Prigozhin na viongozi 35 wa Wagner walipokea mwaliko wa kuhudhuria mkutano huo huko Moscow, siku tano baada ya uasi kusitishwa.
Kulingana na Peskov, Prigozhin alimhakikishia Putin uaminifu wa vikosi vya Wagner bila masharti.
Lakini tusichojua ni nini hasa kilifanyika katika mkutano huu? Hata hivyo, kutokana na kile kilichotokea baada ya mkutano huu, inaweza kusemwa kuwa hapakuwa na "mkataba wa maridhiano" kati ya pande hizo mbili.
Katika siku za hivi karibuni, majukwaa ya vyombo vya habari vya Kirusi yamekuwa yakifanya kazi usiku na mchana ili kuharibu picha ya Prigozhin.
Picha zilivujishwa kwenye majukwaa haya, yawezekana zilichukuliwa wakati wa uvamizi wa jumba la Prigozhin huko St. Petersburg. Picha zinaonyesha michi ya dhahabu na silaha.
Ripoti iliyotangazwa kwenye televisheni ya serikali ya Urusi, ilisema Prigozhin, "si Robin Hood kama anavyojaribu kujionyesha; badala yake, ni mfanyabiashara mwenye historia ya uhalifu huko zamani. Miradi yake mingi ni ya shaka na si ya kisheria."
Na vipi kuhusu makubaliano yaliyofikiwa kati ya Kremlin na Wagner kumaliza uasi mnamo Juni 24?
Kulingana na makubaliano hayo, Prigozhin alitakiwa kuondoka kwenda Belarusi, akifuatana na rafiki yake yeyote wa Wagner ambaye alitaka kuandamana naye.
Fastestsmm ilifuatilia ratiba ya ndege ya Prigozhin ilipopaa kuelekea Belarus mwishoni mwa mwezi uliopita, kabla ya kurejea Urusi siku hiyo hiyo.
Lakini Rais wa Belarus, Alexander Lukashenko, wiki iliyopita alikanusha uwepo wa kiongozi wa Wagner na washirika wake huko Belarus.
Kwa hivyo wako wapi mamluki wa Wagner? Na kiongozi wao Prigozhin yuko wapi? Na nini mipango yao? Na walikubaliana nini na Putin?
Kinachoweza kusemwa kwa sasa ni kwamba inabidi tufuatilie kwa karibu kile ambacho tamthilia hii ya kirusi yenye msisimko itafichua - Uasi wa Juni na Kremlin.
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser. The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.