Kapteini mzoefu amelalamika kuwa licha ya watu – wakiwemo mawaziri wa serikali na raia wa kawaida kufariki, hakuna mipango ya kutosha ya kupunguza hatari ya ajali za helikopta nchini Nepal.
Marubani wanasema uduni wa miundombinu na rasilimali za kutosha za utabiri wa hali ya hewa katika nyanda za juu hufanya safari za kupaa katika maeneo hayo kuwa na changamoto.
Kwa mujibu wa ripoti ya usalama wa anga ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga, zaidi ya watu 85 wamepoteza maisha katika ajali za helikopta nchini Nepal hadi 2019. Tangu kuchapishwa kwa ripoti mwaka 2019, maelezo ya ajali kadhaa za helikopta bado hayajachapishwa na shirika hiyo.
Ajali ya mwanzo kabisa ya helikopta katika rekodi za mamlaka – ilitokea 1989 huko Langtang na watu sita walifariki.
Ajali ya 2006 katika mji wa Ghunsa ilikuwa mbaya zaidi katika historia ya ajali za helikopta nchini Nepal. Timu iliyojumuisha Waziri wa Misitu na Uhifadhi, Gopal Rai, wakisafiri ili kushiriki mpango wa uhifadhi wa wanyamapori ilipata ajali; watu wote 24 walifariki.
Mnamo Februari 2019, watu saba, pamoja na waziri wa utalii wa wakati huo Ravindra Adhikari, walifariki katika ajali ya helikopta huko Pathibhara.
Kamati iliyoundwa kwa ajili ya uchunguzi baada ya ajali hiyo ilieleza – ajali ilisababishwa na hali mbaya ya hewa na uzembe wa rubani katika tathmini yake. Baada ya ajali hiyo, sheria ilipitishwa kuwa ni watu sita tu wanaoweza kubebwa kwenye helikopta za aina hiyo kwenda maeneo ya milima mirefu, badala ya watu saba.
Kipi kinachangia?
Kulingana na Budhisagar Lamichhane, katibu wa Wizara ya Usafiri wa Anga na Utalii, ambaye alifanya kazi katika kamati ya uchunguzi wa ajali ya helikopta ya Pathibhara na ajali zingine, hali mbaya ya hewa na uzembe wa marubani katika kutathmini hali ya hewa ni sababu kuu za ajali hizo.
Lamichhane anasema kuwa jiografia ya Nepal haiwezi kulaumiwa kwa sababu helikopta husafiri kulingana na jiografia nchi. Anaeleza, “jiografia haiwezi kulaumiwa kwa njia yoyote. Hatuwezi kubadili jiografia, tunatakiwa kuruka salama kulingana na jiografia,” anasema.
Wataalamu wanasema marubani wanapaswa kufanya maamuzi kwa kuzingatia sheria na uzoefu.
“Hali ya hewa katika nyanda za juu inabadilika. Kwa sababu hiyo, kuna shuruti ya kuruka ikiwa unaweza kuona mbele,” Lamichhane anaeleza.
Hata hivyo, rubani mmoja mwenye uzoefu anasema – hali ya hewa haitabiriki kutokana na jiografia ya nchi.
Kapteni Shailendra Basnet, ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya kutoa huduma binafsi ya Mountain Helicopters, anasema hakuna miundombinu ya kutosha kwa ajili ya utabiri wa hali ya hewa katika maeneo ya milimani.
Juhudi
Maafisa wanadai kuwa Mamlaka ya Usafiri wa Anga inashughulikia kujenga miundombinu muhimu kwa usalama wa anga nchini Nepal. Kamera zimewekwa kwenye baadhi ya njia za safari katika eneo la Everest ili kutoa taarifa kuhusu hali ya hewa. Picha zilizonaswa na kamera zinapatikana kwa umma.
Lakini kutokana na kukosekana kwa intaneti, picha zinazopatikana kutoka katika kamera hizo haziwezi kuonekana kila mahali, anasema Kapteni mzoefu Basnet. Anashauri kuwa, kamera hizo zinapaswa kuwekwa katika sehemu nyingi zaidi.
Basnet alieleza, kwa taarifa ya hali ya hewa mtu hutegemea vyanzo vya kigeni vya mtandaoni vinavyotoa taarifa za utabiri wa hali ya hewa kwa safari za ndege kwenda maeneo mengi.
“Tunapokwenda baadhi ya maeneo inatubidi tuwapigie wenyeji na kuwauliza hali ya hewa ikoje, kuna mawingu au hakuna,” alisema.
Anadhani ikiwa Nepal inaweza kupata taarifa za hali ya hewa ambazo India na China hupata kutoka katika satelaiti, itasaidia kufanya safari za helikopta katika maeneo ya milimani kuwa salama zaidi.
Ajali nyingi hutokea wapi?
Kati ya ajali tatu za helikopta ambazo zimetokea nchini Nepal katika miezi michache iliyopita, mbili zimetokea katika maeneo ya nyanda za juu na Himalaya. Aprili iliyopita, ndege ya Heli Everest ilianguka katika eneo la Dhaulagiri na ndege ya Simric Air ilianguka Sankhuwasabha mwezi Mei.
Kulingana na ripoti ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga, ajali nyingi za helikopta zilitokea katika wilaya za Himalaya na kulingana na wataalamu, utabiri wa hali ya hewa katika mkoa huo sio rahisi.
Katika miaka kumi iliyopita nchini Nepal, matumizi ya helikopta kwa uchunguzi wa milima, usafiri na uokoaji yameongezeka.
Baadhi ya ajali mbaya tangu 2006
• Aprili 2019 – Takriban watu watatu waliuawa wakati helikopta ya Summit Air ilipogongana na helikopta mbili karibu na njia ya kurukia ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa Lukla katika Wilaya ya Solukhumbu.
• Februari 2019 – Watu saba, akiwemo Waziri wa Utamaduni, Utalii na Usafiri wa Anga wa wakati huo Rabindra Adhikari, walikufa wakati helikopta ya Nasaba ilipoanguka karibu na Pathibhara huko Taplejung.
• Septemba 2018 – Helikopta ya Altitude Air iliyokuwa ikitoka Gorkha kuelekea Kathmandu ilianguka katika msitu kati ya Dhading na Nuwakotbir. Mtalii wa Kijapani na wengine watano walikufa
• Mei 2015 – Wanajeshi sita wa Marekani, maafisa wawili wa jeshi la Nepal na raia watano walifariki wakati helikopta ya Jeshi la Marekani iliyokuwa katika shughuli za kutoa msaada baada ya tetemeko la ardhi na shughuli za uokoaji kuanguka karibu na Charikot.
• Juni 2015 – Watu wanne walikufa wakati helikopta iliyokuwa imekodishwa na Madaktari Wasio na Mipaka kwa ajili ya misaada na uokoaji wa tetemeko la ardhi huko Sindhupalchowk ilipoanguka.
• Septemba 2006 – Helikopta ya Sri Air ilianguka Taplejung Ghunsa, Waziri wa Uhifadhi wa Misitu na Ardhi, Gopal Rai, na watu 24 walifariki.
• Mei 2023 – Helikopta ya Simric Air ilianguka Siprung, Sankhuwasabha, na mmoja wa watu waliojeruhiwa aliaga dunia wakati wa matibabu.
#Kwanini #usafiri #helikopta #hatari #nchini #Nepal #Fastestsmm #News #Swahili