Updated News to your hands? Contact Us Join us!
Posts

Mkuu wa Wagner kuhamia Belarus baada ya kuachana na uasi - Fastestsmm Swahili

Mkuu wa Wagner kuhamia Belarus baada ya kuachana na uasi - Fastestsmm Swahili

Copyright: Reuters

Na tunaanzia huko nchini Urusi ambapo matukio mengi yamefanyika ndani ya saa 24 zilizopita tangu kiongozi wa Wagner Yevgeny Prigozhin kuitisha uasi dhidi ya jeshi la Urusi na kisha baadaye kusitisha harakati zake kuelekea Moscow.

Mkuu wa kundi la mamluki la Wagner amepigwa picha na shirika la habari la Reuters akiondoka katika mji wa Rostov-on-Don, ambao wapiganaji wake waliudhibiti mapema jana.

Yevgeny Prigozhin alikuwa akiendesha gari kutoka makao makuu ya jeshi ya wilaya jijini, shirika hilo linasema.

Kulingana na vyombo vya habari vya serikali ya Urusi, Progozhin ataondoka Urusi kuelekea Belarus na mashtaka yote dhidi yake na vikosi vyake vya Wagner yatafutwa na mamlaka ili kuepusha "umwagaji damu".

Yevgeny Prigozhin na askari wake hawatashtakiwa, inasema Kremlin. Wapiganaji wa Wagner wameripotiwa kuanza kuondoka katika mji wa kusini wa Rostov-on-Don ambako uasi wao ulianza. Prigozhin alitoa wito wa uasi dhidi ya jeshi la Urusi - na vikosi vyake vilikamata Rostov, kituo kikuu cha kijeshi.

Wenyeji wa Rostov wawashangilia kuunga mkono wapiganaji wa Wagner

Copyright: Reuters

Wakati wapiganaji wa Wagner wakiondoka katika makao makuu ya kijeshi huko Rostov-on-Don, wakazi wa jiji hilo wamekuwa wakiimba "Wagner! Wagner!" katika onyesho dhahiri la kuunga mkono mamluki.

Usiku ulipoingia, watu kadhaa wa eneo hilo walikusanyika kuwaonyesha wapiganaji hao uungwaji mkono kulingana na picha kutoka jiji hilo.

Haijabainika iwapo walikuwa wakionyesha kuunga mkono hatua za wapiganaji hao nchini Ukraine au uasi uliozuiliwa.

Je, huu ndio mwisho wa Prigozhin na Wagner?

Copyright: Reuters

Yevgeny Prigozhin kuhamia Belarus na wapiganaji wa Wagner kuingizwa katika jeshi la Urusi kunaweza kumaanisha mwisho kundi hilo la mamluki, mtaalam ameiambia Fastestsmm.

Andrew D'Anieri, kutoka taasisi ya wataalam ya Baraza la Atlantiki yenye makao yake nchini Marekani, anasema ni vigumu kusema nini hasa kitakachotokea, kutokana na hali ya mkanganyiko na isiyoeleweka ya taarifa zinazotoka Urusi.

Lakini pia anasema kuanguka kwa kwa Wagner haimaanishi kwamba makampuni yote ya kijeshi ya kibinafsi nchini Urusi "yako nje pia".

"Ingawa kiufundi ni kinyume cha sheria nchini Urusi, tumeona ongezeko la makundi hayo katika kipindi cha miezi 12 hivi."

D'Anieri anasema imekuwa wazi katika siku ya mwisho "ni kiasi gani kundi la kufanya maamuzi ni ndogo huko Moscow" na jinsi mamlaka ya Vladimir Putin ni dhaifu.

‘Ikiwa uliwafuata waenezaji wa propaganda wa Kremlin kwa karibu ... kulikuwa na ukimya mwingi na bila kujua la kufanya, kwa sababu kwa kweli hapakutolewa uamuzi uliofanywa kuhusu jinsi ya kujibu."

Unaweza pia kusoma

Saa 24 za jaribio la uasi Urusi

Mkuu wa Wagner kuhamia Belarus baada ya kuachana na uasi

Je, haya ni mapinduzi? Prigozhin anafanya nini nchini Urusi?

Kiongozi wa kundi la Wagner aapa kuwapindua viongozi wa kijeshi wa Urusi

Tazama: Mamluki wa Wagner wenye silaha katika mitaa ya Rostov

[ad_2] #Mkuu #Wagner #kuhamia #Belarus #baada #kuachana #uasi #Fastestsmm #Swahili
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.