Jioni Julai 2022 yenye joto , baridi iliwaingia wachezaji wa Juventus huko mjini. Miaka sita baada ya kuondoka kwenda Manchester United, Paul Pogba alitangaza kurejea katika jiji hilo.
Kwa mashabiki, kile kinachoitwa ‘Pogback’ kiliwakilisha kurejea kwa maisha ya furaha – kwa timu ya kitambo ambayo ilishinda mataji manne ya nyumbani mfululizo na kufika fainali mbili za Ligi ya Mabingwa mnamo 2015 na 2017.
Mfaransa huyo alingaa kwenye mechi ya kwanza, ambapo alikamilisha mpangilio mzuri wa safu ya kati na Andrea Pirlo, Claudio Marchisio na Arturo Vidal.
Siku iliyofuata, mashabiki walishuka kwenye kituo cha JMedical kumkaribisha Pogba na mchezaji mwingine mpya, Angel di Maria mwenye umri wa miaka 34.
Kurudi kwao kulikua kumekamilika: Kocha Massimiliano Allegri na kiungo wa kati Pogba wangeirudisha klabu katika utukufu wa Ulaya, jambo ambalo hata Cristiano Ronaldo alishindwa kutimiza.
Licha ya baadhi ya watu kuthubutu kusema wachezaji wa kiwango na umri huo wangekuja tu Juventus kufanya mazoezi ya Kombe lijalo la Dunia huko Qatar, jua liliangaza Turin, sio tu kwa njia ya sitiari.
Rais Andrea Agnelli alikuwa bado kwenye usukani, Juventus walikuwa wakitunishiana misuli baada ya kukosa mataji mfululizo ya Serie A kwa vilabu vya Milan, na mashabiki walitamani mataji.
Miezi 12 mbele baadaye na matarajio ya siku hiyo ya kiangazi.
Ulikuwa mlima mkubwa kuupanda
Kurudi kwa Pogba kulikuwa janga tangu mwanzo.
Alijeruhiwa goti lake la kulia wiki mbili baada ya kuwasili kwenye ziara ya maandalizi ya msimu mpya nchini Marekani.
Licha ya kushauriwa kufanyiwa upasuaji, kwa matumaini ya kushiriki Kombe la Dunia badala yake alichagua kufanyiwa gusa gusa ya mganga.
Hatahivyo ganga ganga hiyo haikufaulu
Upasuaji uliohitajika mwezi Septemba ulimlazimu kuikosa Qatar na kuwatazama wachezaji wenzake wa Ufaransa wakipoteza mchezo wa fainali dhidi ya Argentina kutoka jukwaani.
Mkazo zaidi wa misuli ulimweka nje hadi Februari 28, aliporejea kama mchezaji wa akiba katika mechi ya derby ya Turin.
Pogba kisha alitolewa kwenye mechi ya Juventus ya Ligi ya Europa dhidi ya Freiburg mwezi Machi kwa sababu za kinidhamu, na alivumilia tatizo lingine alipopata jeraha la paja kwa kupiga mipira ya adhabu akiwa mazoezini.
Baada ya kurejea katika utimamu wa mwili, alifurahia mechi za kutia moyo dhidi ya Atalanta katika Serie A na Sevilla kwenye Ligi ya Europa mwezi Mei, na hatimaye alikuwa tayari kufurahia nafasi ya kuanza – siku 390 baada ya kufanya hivyo mara ya mwisho ikiwa Manchester United ilipochapwa 4-0 na Liverpool kwenye Uwanja wa Anfield tarehe 19 Aprili 2022.
Wakati Juventus ilipomenyana na Cremonese mnamo 14 Mei kwenye Uwanja wa Allianz, ulikuwa usiku ambao ulikusudiwa kumsaidia Pogba kuweka miezi ya matatizo yake nyuma.
Uwanja ukapendezwa na kurejea kwake, akaitikia kwa kichwa na kuwakonyeza wenzake jicho huku akipasha moto misuli.
‘Pogba aliyerudi’ alicheza dakika 24 pekee
Kuanza kwa Pogba kwa mara ya kwanza ndani ya zaidi ya mwaka mmoja kulichukua dakika 24 pekee
Baada ya dakika 24 tu, huzuni ya maumivu ilifuatiwa na hali ya kutokuamini iliyokuwa kwenye uso wa Pogba – machozi yalitiririka mashavuni mwake alipokuwa akiondoka.
Uwanja mzima ulipigwa na butwaa – mashabiki hawakuamini walichokuwa wakikiona. Walimpenda sana; walimkaribisha Pogba akiwa kijana asiyejulikana ambaye alikomaa na kushinda mataji, aliondoka akiwa nyota na kurejea akiwa bingwa wa dunia.
Miezi tisa baada ya kuvamiwa na kukaribishwa na kundi la watu katika kituo cha matibabu cha Juve, alirudi huko bila nguvu za kupiga picha za selfie. Utambuzi wa daktari ulibaini kwamba alikuwa amepata jeraha la misuli na hivyobasi asingeweza kucheza msimu wote uliosalia.
“Paul ni mwanamue, ana mabega mapana na tunamsubiri,” Allegri alisema baada ya mchezo huo.
‘Pogback’ alifikia dakika 108 katika mechi sita za Serie A, mechi tatu na asisti moja kwenye Ligi ya Europa, na dakika 11 kwenye Coppa Italia – jumla ya dakika 161 bila kufunga bao.
Akiwa na mshahara mkubwa zaidi wa wachezaji wote wa Juve, Pogba ameigharimu klabu hiyo takriban pauni 56,000 kwa dakika msimu huu.
“Hatutamwacha. Tunamsubiri na tunamwamini, vinginevyo hatukumpa mkataba wa miaka minne,” afisa mkuu wa soka wa Juventus Francesco Calvo alisema miezi michache iliyopita.
Je, anaweza kupona hivi karibuni?
Kumekuwa na mazungumzo kati ya mashabiki kwamba Pogba anapaswa kupunguza mshahara wake kwa hiari. Hata hivyo, licha ya kujaribu kuepuka upasuaji majira ya joto yaliyopita, hakuwa na bahati na majeraha yake.
Kwa hakika, amezungumza hivi majuzi kuhusu jinsi anavyohisi matatizo yake mengi ya kimwili yalitokana na jinsi alivyokuwa akihisi kiakili.
“Unapokuwa hauko vizuri kichwani, mwili unafuata,” kijana huyo mwenye umri wa miaka 30 aliliambia jarida la Ufaransa Views.
“Nilikuwa na msongo wa mawazo, mwili wangu ulikuwa na wasiwasi. Na nilitaka sana kurudi haraka, kucheza na kuonyesha watu, kunyamazisha kila mtu .”
Matatizo ya majeraha ya Pogba yanarudi nyuma zaidi ya mwaka uliopita – katika misimu yake sita akiwa na Manchester United alikosa zaidi ya mechi 100.
Lakini mustakabali wake wa hivi karibuni unaonekana kuwa Juventus. Je, ni klabu gani itacheza pata potea na kumlipa mshahara wake mkubwa?
Huku mkataba wa Pogba ukikamilika tarehe 30 Juni 2026, jambo pekee la kweli la kufanya ni kutazamia, kujaribu kusahau kilichotokea na kuanza upya.
Hata hivyo, kuna hisia kwamba mambo mengi yametokea tangu alipoondoka Juventus mwaka 2016 – upasuaji mara mbili kwenye kifundo cha mguu wa kulia na goti, kaka yake anachunguzwa kwa madai ya njama ya kumnyang’anya pesa, na mfululizo wake wa kusikitisha wa majeraha na kurudi kwa muda mfupi. .
Anachohitaji Pogba ni kurejeshwa upya kabisa, kimwili na kiakili, lakini kinachobakia akilini mwa mashabiki wa Juventus ni machozi yale dhidi ya Cremonese na iwapo kupona kamili kunawezekana.
#Paul #Pogba #Machozi #matatizo #Turin #mwaka #ambao #hatawahi #kuusahau #tangu #aliporudi #Juventus #Fastestsmm #News #Swahili