Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 07.07.2023: Onana, Hojlund, Caicedo, Bonucci, Timber, Hojbjerg - Fastestsmm News Swahili
Chanzo cha picha, Getty Images
Kipa wa Inter Andre Onana
Manchester United wanakaribia kumsajili kipa wa Inter Andre Onana, 27, baada ya kuafikiana na mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon. (Fabrizio Romano)
The Red Devils pia wanapanga kumnunua mshambuliaji wa Atalanta na Denmark Rasmus Hojlund, 20 kwa pauni milioni 50. (Telegraph).
Chelsea italazimika kulipa zaidi ya pauni milioni 100 ikiwa wanataka kumsajili kiungo wa Brighton na Ecuador Moises Caicedo, 21, msimu huu wa joto (Telegraph).
Newcastle wanajiandaa kumnunua beki mkongwe wa Italia na Juventus Leonardo Bonucci, 36, ili kuongeza uzoefu katika kampeni yao ijayo ya Ligi ya Mabingwa. (TEAMtalk)
Chanzo cha picha, Reuters
Jurrien Timber wa Ajax atafanyiwa vipimo vya afya Arsenal siku ya Ijumaa huku The Gunners wakiwa na uhakika wa kukamilisha dili la pauni milioni 38.5 kwa ajili ya beki huyo wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 22. (Standard).
Kiungo wa Tottenham Ivan Perisic amemwambia mkufunzi Ange Postecoglou kwamba ana nia ya kusitisha mkataba wake, huku Mcroatia huyo mwenye umri wa miaka 34 akitaka kujiunga na Hajduk Split. (Gianluca Di Marzio)
Wakati huo huo, Atletico Madrid wamewasiliana na kiungo wa Spurs na Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, 27, ambaye pia amekuwa akihusishwa na uhamisho wa Bayern Munich. (Mail)
Chanzo cha picha, Tottenham Hotspur FC via Getty Images
Kiungo wa Spurs na Denmark Pierre-Emile Hojbjerg
Southampton wanaamini kuwa watapewa bei inayotakiwa ya pauni milioni 50 wanapojiandaa kumnunua kiungo wa kati wa Ubelgiji Romeo Lavia, 19, huku Chelsea, Liverpool na Arsenal pia wakiwania saini yake. (Sky Sports)
Matumaini ya Crystal Palace kumnunua tena Wilfried Zaha, 30, yamefifia huku mshambuliaji huyo akizingatia ofa kutoka kwa Lazio, Fenerbahce na Al-Nassr. (Standard)
Fulham wanakaribia kufikia mkataba mpya na mchezaji huru Willian baada ya mshambulizi huyo wa Brazil, 34, kuwa mchezaji huru mwishoni mwa juma lililopita. (The Athletic - usajili unahitajika)
Chanzo cha picha, Reuters
Mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha huenda akahamia klabu nyingine
Beki wa Arsenal Mfaransa William Saliba, 22, ametia saini mkataba mpya utakaomweka Emirates Stadium hadi 2027. (The Athletic - usajili unahitajika)
West Ham wanafikiria kumsajili kiungo wa Juventus Denis Zakaria. The Hammers kwanza wanaweza kumchukua kwa mkopo mchezaji huyo wa kimataifa wa Uswizi mwenye umri wa miaka 26 na chaguo la kumnunua kwa £15.4m. (Standard)
The Hammers pia wanavutiwa na wachezaji wa Joao Palhinha, 27, wa Fulham na James Ward-Prowse wa Southampton mwenye umri wa miaka 28 wanapokiandaa kuimarisha kikosi chao . (Guardian)