Uthibitisho kwamba wafanyakazi waliokuwa ndani ya nyambizi ndogo ambayo ilitoweka wakati wa kupiga kwenye ajali ya Titanic karibu wiki moja iliyopita wamekufa wote ina maana kwamba operesheni kubwa ya utafutaji iliyoanzishwa katika maji ya Bahari ya Atlantiki inapewa vipau mbele vipya kwa sasa.
Walinzi wa Pwani wa Marekani walithibitisha siku ya Alhamisi alasiri kwamba wanaume wote watano waliokuwa ndani ya nyambizi hiyo walikufa kufuatia kile ambacho huenda kilikuwa “msiba mbaya” wa nyambizi ndogo kutoka kampuni ya OceanGate inayoendesha safari za kitalii katika eneo ilikozama meli ya Titanic
Lakini maswali mengi kuhusu kile kilichotokea yanabaki bila kujibiwa na kutafuta majibu ni njia mojawapo ya kusonga mbele.
Je, miili itapatikana?
Mkuu wa kikosi cha walinzi wa pwani ya Marekani John Mauger amesema hakuweza kuthibitisha kama Walinzi wa Pwani wa Marekani wataweza kupata miili ya waathiriwa wa tukio hilo au la
“Haya ni mazingira ya kusikitisha mno ,” alisema.
Waliokuwemo ndani ya nyambizi hiyo walikuwa wafanyabiashara matajiri wa Uingereza Hamish Harding na Shahzada Dawood, ambaye mtoto wao Suleman alijiunga naye kwenye nyambizi ya Titan.
Mkurugenzi Mtendaji wa OceanGate Stockton Rush pia alikuwa sehemu ya wafanyakazi, pamoja na mtaalamu wa kupiga mbizi wa zamani wa jeshi la wanamaji wa Ufaransa Paul-Henry Nargeolet.
Nini hasa kitatokea kwa zoezi la utafutaji?
Haijabainika wazi kufikia sasa ni chombo gani kitaongoza uchunguzi kwa vile hakuna itafaki maalum inayofuatwa katika eneo la maji ya chini.
Mkuu wa kikosi cha walinzi wa pwani ya Marekani John Mauger alisema ilikuwa ni vigumu hasa kwa sababu tukio hilo lilifanyika katika sehemu ya mbali ya bahari, iliyohusisha watu wa mataifa tofauti.
Lakini baada ya kuchukua jukumu kuu katika operesheni hiyo hadi sasa, Walinzi wa Pwani ya Merekani wanaweza kuendelea kuwa na sehemu muhimu kwenye zoezi la uokoaji.
Mauger ameongeza kuwa wataendelea kuchunguza vifusi na vyombo kadhaa,huku wafanyikazi wa Afya na mafundi watalazimika kubaki kwenye eneo la tukio.Na vikosi maalum kuondoka katika muda wa saa 24 zijazo.
Magari ya uendeshaji ya mbali (ROVs) yanayofanya kazi baharini karibu na eneo iliopo meli ya Titanic pia yatabaki kwa muda kadhaa
“Sina ratiba ya lini tutanuia kusimamisha shughuli za mbalimbali za baharni kwa wakati huu,” alisema John Mauger mkuu wa kikosi cha walinzi wa Marekani.
Vipi kuhusu mabaki ya Nyambizi hiyo ndogo ?
Itakuwa muhimu kukusanya vipande vingi iwezekanavyo, ikiwa ni pamoja na vipande vya nyuzi za kaboni ambazo zilitumika kutengeza chombo hicho ili mamlaka husika iweze kupata picha kamili ya kile kilichotokea.
Juhudi zinaendelea kuchora ramani ya eneo ambalo sehemu za Titan zilipatikana.
Paul Hankin, mtaalam wakupiga mbizi katika bahari ya chini, alielezea kuwa zoezi la utafutaji hadi sasa umepata vipande vitano sasa uchunguzi utafanywa ili kuthibitisha kuwa ni nyambizi ndogo iliyopotea.
Maafisa wanasema vipande vitano vikubwa vilipatikana pamoja na mabaki karibu na meli ya Titanic.
Miongoni mwao, ni pamoja na pua ya nyambizi hiyo.
Tukio hilo litachunguzwa vipi?
Mkuu wa kikosi cha walinzi wa pwani ya Marekani John Mauger alisema serikali za nchi zilizohusika katika tukio hilo zimekuwa zikikutana ili kujadili namna ambavyo uchunguzi unaweza kuendeshwa.
Wale wanaohusika katika uchunguzi wowote watakuwa wakitafuta kuthibitisha nadharia kwamba mlipuko ulisababisha vifo vya waliokuwa ndani ya Titan na, ikiwa ndivyo, lini na kwa nini ilitokea.
Mkuu huyo aliongeza kuwa ingawa wigo wa hii ulikuwa nje ya majukumu yake, maswali mapana kuhusu kanuni na viwango vya zoezi hilo la bahari ya chini ya maji yanaweza kuwa lengo la mapitio ya baadaye.
Chanzo kingine cha habari kuhusu kile kilichotokea kwa nyambizi ya Titan kinaweza kuwa – maikrofoni ya chini ya maji ambayo hutumiwa kusikiliza majaribio haramu ya silaha za atomiki.
Haya yalisaidia kubaini kuwa manowari ya Argentina San Juan ilikuwa imevamia baada ya kutoweka kwenye pwani ya nchi hiyo mnamo mwaka 2017.
Huenda maikrofoni hizo zilirekodi hatua za mwisho wa nyambizi ya kampuni ya Oceangate Titan na zinaweza kutoa taswira ya muda kamili ya wakati ambao mkasa huo ulitokea.
Jeshi la Wanamaji la Marekani liligundua sauti “zinazoendana na milipuko” muda mfupi tu baada ya nyambizi ya Titan ya kampuni ya OceanGate kupoteza mawasiliano, afisa wa jeshi la wanamaji alisema.
#Nini #kinachofuata #baada #nyambizi #ndogo #Titan #kutoweka #Fastestsmm #News #Swahili