
Oleh alishambuliwa mgogoni
- Author, Andrew Harding
- Nafasi, Fastestsmm News
Dawa ya ganzi ilipoanza kuisha, yule askari wa Ukraine – kijana wa miaka 19 aliyejaa matope, alitoa sauti ndogo nyuma ya gari la wagonjwa, kisha akapapasa barakoa yake ya oksijeni na kusema huku akigugumia, "nipe bunduki yangu."
"Mara nyingi huwa ni maumivu makali namna hii," alisema Dkt. Inna Dymitr, akipapasa uso uliopauka wa askari katika gari la wagonjwa likitembea kwa kasi mbali na mstari wa mbele kusini-mashariki mwa Zaporizhzhia.
Jina la askari huyo kijana ni Oleh. Asubuhi hiyo kombora kutoka Urusi lilipiga karibu yake na kuchimbua shimo kubwa.
"Ni askari imara, lakini yuko katika hali mbaya, na tunapata wengi kama yeye," alisema Dkt. Dymitr, akiorodhesha kesi nyingine kama hiyo ya siku za hivi karibuni. Anafanya kazi katika kikundi binafsi cha msaada kinachofadhiliwa na nchi za magharibi, kiitwacho MOAS.
Majeruhi kutoka kwenye mlima eneo la kujibu mapigo mashambulizi ya Urusi. Katika ziara ya nadra kwenye sehemu hii - baadhi ya askari na wafuatiliaji wana mashaka ikiwa kuna mafanikio yatafikiwa, au labda safu za ulinzi za Urusi ni imara sana.
"Bila msaada zaidi [wa Magharibi], nadhani tunaweza kupoteza vita hivi," alisema Kyrylo Potras, mwanamaji wa Ukraine ambaye mguu wake wa kushoto ulikatika kutokana na bomu la chini ya ardhi la Urusi mwaka 2020.
Kwa sasa amerejea mstari wa mbele na anasema, uwepo wa mabomu ya chini ya ardhi ni kikwazo kikubwa. "Warusi wako wengi. Wana bunduki nyingi za kuzuia vifaru na mifumo ya makombora," alisema.
Baada ya mwezi mmoja tangu mashambulizi ya kujibu mapigo yaanze, kuna askari wengi na wafuatiliaji wa mambo hawakubaliani kwamba hatua ya awali ya kujibu mapigo inakwenda kama ilivyo pangwa.
Mashambulizi ya mstari wa mbele – katika eneo lenye ukubwa wa zaidi ya kilomita 1,000 (maili 620) kutoka Pwani ya Bahari Nyeusi hadi kaskazini-mashariki mwa Ukrainia na Urusi - kamwe ngome za Urusi hazitavunjwa kirahisi kama ambavyo jeshi la Ukraine lilivyofanikiwa mwaka jana.
Artem mwanajeshi wa Ukraine
Nadharia za kuvunja ngome za Urusi
Baada ya kutumia wiki chache zilizopita kutembelea sehemu tatu tofauti za mstari wa mbele na kuzungumza na watu mbalimbali, mitazamo inagawika katika makundi matatu.
Nadharia ya kwanza – hii ilielezwa kwa mara ya wiki mbili zilizopita, na daktari aliyechoka niliyekutana naye katika hospitali nje ya mji wa Donbas huko Bakhmut.
Wakati mashambulizi na makombora yakitamalaki, alielezea vifo vinaongezeka vya wanajeshi wa Ukraine, na kuonya kwamba Urusi ilikuwa na muda mrefu sana kuandaa ulinzi wake na ina wanajeshi wengi.
Akahitimisha kwamba wakati Ukraine inaweza kuwarudisha nyuma Warusi hata kwa makumi ya kilomita, itakuwa vigumu kwao kufanya zaidi kwa sababu ya umiliki wa kimkakati wa Urusi wa mashariki na kusini-mashariki mwa Ukraine.
"Nadhani vita hivi havitasuluhishwa katika uwanja wa vita. Vitamalizika kwa makubaliano ya kisiasa," alisema kwa huzuni.
Nadharia ya pili- ni wale wanao amini kuna uwezekano wa kuharibu mstari wa mbele wa Urusi, ingawa hautoondoka wote. Hii nilielezwa wakati wa safari ya masaa matatu kusini magharibi kwa Bakhmut, mbali na mji wa mdogo wa Velyka Novosilka.
Katika safu ya milima iliyopangana kuelekea Bahari Nyeusi, vikosi vya Ukraine vilikuwa vikisonga mbele, vikitafuta njia kupitia maeneo yenye mabomu ya ardhini na kushambulia nafasi za Urusi kutoka pembe zisizotarajiwa, na polepole, kukamata sehemu za wilaya na vijiji kadhaa na miji midogo. .
"Mimi naangalia uhalisia, ingawa baadhi ya watu hudhani nakata tamaa," Artem, mwanajeshi mwenye umri wa miaka 36, alisema wakati ndege ya Ukraine ikiunguruma. Maoni yake yalikuwa kwamba ari ya askari wa Urusi ilikuwa chini, na Ukraine ilikuwa na uwezo wa kupata mafanikio makubwa katika miezi ijayo.
Nadharia ya tatu - maoni - ambayo yanashikiliwa na wachambuzi mashuhuri wa kijeshi wa nchi za magharibi kama Mick Ryan na majenerali kama mkuu wa vikosi vya jeshi la Uingereza, Sir Tony Radakin - kwamba uvamizi uko kwenye hatua. Na baada ya wiki, au miezi, ulinzi wa Urusi utasambaratika, ikiruhusu Ukraine kuteka eneo muhimu la kimkakati na kusonga mbele karibu (ikiwa sio ndani) ya Peninsula ya Crimea.
Wafuasi wa nadharia hii wanahimiza uvumilivu, na sio kukata tamaa, wakisema ukosefu wa mashambulizi ya anga ya Ukraine inamaanisha haiwezi kufanya kazi muhimu ya mapema ya kuharibu mifumo y Urusi - ikimaanisha vituo vyake vya usambazaji wa vifaa na vituo vya kamandi - kwa kasi ambayo ingetaka.
Badala yake, vikosi vya Ukraine vinatumia makombora ya ardhini kufanya kazi hiyo, na wakati huo huo kushambulia maeneo ya Urusi katika sehemu nyingi iwezekanavyo ili kuharibu nguvu kazi na vifaa vya adui.
"Zuia chakula, jitanue kieneo na shambulia," ndivyo Sir Tony, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Uingereza, alielezea mkakati huo wiki hii, akihitimisha kwamba Urusi tayari imepoteza karibu nusu ya ufanisi wa wa jeshi lake.
Katika hospitali ambapo Oleh, askari mwenye umri wa miaka 19 aliyekuwa na jeraha kubwa la mgongo aliwekwa bendeji kwa muda mfupi kabla ya kupata usafiri wa gari la wagonjwa kumchukua; Daktari wa Ukraine ambaye aliomba tutumie jina lake la kwanza tu, Yevhen, anasema,
"Kila mtu anasubiri [mafanikio]. Tunaamini na kusubiri. Tunajua kila kitu kitakuwa sawa. Tunahitaji tu kuwa na subira," alisema kwa tabasamu, akiwa ameketi kwenye mwanga wa jua nje ya hospitali pamoja na kuongezeka kwa milio ya silaha zinazosikika kwa mbali.